Je, Nitahamisha Vipi Umiliki wa Zana na Vifaa Vyangu vya Starlink? (Akaunti za Makazi na Biashara)
Taarifa Muhimu Kabla ya Kuhamisha Zana na Vifaa vya Starlink
- **Wajibu **: Starlink haiwajibikii hali ya seti zinazouzwa au kuhamishwa na wahusika wengine.
- Malipo: Hakikisha maagizo na huduma zote zinalipiwa kikamilifu, bila kukuwepo kwa deni lolote.
- Ghairi Huduma: Lazima ughairi huduma yako ili uhamishe zana na vifaa.
- ** Kukomeshwa kwa Huduma **: Mara baada ya kuhamishwa, Starlink huondolewa kwenye akaunti yako kabisa. Huduma itakomeshwa mara moja na siku zozote za huduma zilizobaki zitapotea.
- ** Kujisajili kwa Mtumiaji Mpya**: Mmiliki mpya ni lazima ajisajili kwa huduma kupitia starlink.com. Upatikanaji unaweza kutofautiana kulingana na eneo na aina ya huduma (kwa mfano, huduma ya Makazi, huduma ya Ughaibuni, n.k.).
- Malipo: Mtumiaji mpya atatozwa kwa mwezi wa kwanza wa huduma baada ya kuamilishwa.
- Dhamana: Dhamana inategemea tarehe asili ya ununuzi, hata ikiwa imeuzwa au kuhamishwa na mhusika mwingine. Thibitisha hali ya seti kabla ya kununua kutoka kwa wahusika wengine. Pata maelezo zaidi kuhusu udhamini hapa.
- ** Utekelezaji wa Nchi **: Seti za Starlink zinapewa vyeti kwa nchi mahususi. Baadhi ya huduma zinaweza kuzuiwa kulingana na nchi ya ununuzi wa awali.
- Vizuizi vya Kuhamisha:
- Kuhamisha hakuruhusiwi hadi siku 120 baada ya kununua au siku 90 baada ya kuamilisha, muda wowote utakaotangulia.
- Starlink Mini haiwezi kuhamishiwa kwenye akaunti ya Biashara kwa wakati huu.
- Ikiwa umeanzisha urudishaji wa zana na vifaa vyako na mchukuzi amechanganua lebo, hustahiki kuhamisha zana na vifaa vyako.
- Ikiwa umeanzisha urudishaji lakini mchukuzi hajachanganua lebo, bado unastahiki kuhamisha zana na vifaa vyako.
Kumbuka:
- Ikiwa unatatizika kuhamisha Starlink yako siku 120 baada ya kununua kutoka kwa muuzaji rejareja aliyeidhinishwa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Usaidizi kwa Wateja cha Starlink na uthibitisho wako wa ununuzi.
- Tumejizatiti kutoa intaneti ya kasi ya juu nchini Nigeria na tunashirikiana kwa karibu na wadhibiti ili kufanya marekebisho ambayo yataboresha huduma kwa wateja. Mpaka mabadiliko haya yaidhinishwe, tunasimamisha maagizo mapya ya Makazi. Weka amana sasa ili uhifadhi Starlink yako na utapokea arifa baada ya maagizo kuanza tena.
Jinsi ya Kuhamisha Starlink Yako
- Ingia kwenye akaunti yako ya Starlink kupitia Starlink.com.
- Nenda kwenye "Starlink Zako" kisha ubofye "Dhibiti" karibu na seti ambayo ungependa kuhamisha.
- Bofya "Ghairi Huduma" upande wa kushoto. (Zingatia kitambulishi cha Starlink, kwani hutakiona baada ya kuondolewa kwenye akaunti yako.)
- Chini ya "Vifaa", tafuta Starlink yako, bofya "Hamisha," kisha uthibitishe masharti. Hii huiondoa kabisa kwenye akaunti yako.
- (Hiari) Weka barua pepe ya mmiliki mpya ili kutuma kiungo cha uamilishaji. Ikiwa sivyo, bofya "funga" ili ukamilishe.
- Rejesha mipangilio ya kiwandani ya ruta yako.
- Mpe mmiliki mpya vitu vyote vilivyo kwenye seti.
- Shiriki Kitambulishi cha Starlink na mmiliki mpya ili kuamilisha:
- ** Nambari Tambulishi ya Seti **: Kwenye lebo ya usafirishaji (kwa mfano, KIT00000000). Mfano hapa.
- Nambari Tambulishi ya Sahani: Inatofautiana kulingana na aina ya zana na vifaa:
- Standard/Shirika: Nyuma ya Starlink karibu na tundu la kiunganishi.
- Mini: Upande wa chini kushoto wa Kiweko.
- Standard Otomatiki/High Performance: Chini ya mlingoti.
- Flat High Performance: Nyuma ya Starlink karibu na tundu la kiunganishi.
- **Kitambulisho cha Kifaa **: Fungua programu ya Starlink, nenda kwenye Mipangilio > Ya Kina na utafute kitambulisho chini ya "STARLINK" (k.m., 00000000-00000000-00000000).
Jinsi ya Kuamilisha Starlink Yako
Ikiwa wewe ni mmiliki mpya, amilisha Starlink yako kwa kutembelea Maswali yetu Yanayoulizwa Mara kwa Mara: Ninaweza kuamilisha Starlink yangu vipi?.
Mada Zinazopendekezwa: