Linganisha mipango [hapa] (https://www.starlink.com/service-plans).
Starlink hutoa mipango ya huduma ya maeneo yasiyobadilika na ya mwendoni iliyoundwa kutoa urahisi wa kufanya mabadiliko na kukidhi mahitaji anuwai ya intaneti kwa watumiaji na biashara ulimwenguni. Ukiwa na Starlink, ni rahisi kubadilisha mpango wako, kununua data zaidi na kuongeza maeneo ya ziada ya huduma.
Bei itatofautiana kulingana na soko kwa kutegemea sarafu, kodi na hali nyingine za soko la eneo. Angalia hapa kwa maelezo zaidi. Isitoshe, Starlink haitoi tena mpango wa huduma wa 'Juhudi Bora Zaidi'.
Tafadhali kumbuka: Starlink mara kwa mara inaweza kutoa mipango ya huduma ya promosheni au upatikanaji mdogo kwa wateja fulani. Ofa hizi hazipatikani katika maeneo yote na huenda zisionekane miongoni mwa machaguo ya mpango wa huduma yanayopatikana. Mipango ya huduma inayoonyeshwa kwenye dirisha la 'Dhibiti Mpango wa Huduma' inaonyesha mipango inayopatikana kwa sasa katika eneo lako. Ikiwa mpango hauonekani hapo, huenda hautolewi katika eneo lako kwa wakati huu.
Taarifa Nyingine
Pata taarifa za barua pepe za Starlink hapa.
Mada Zinazohusiana:
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.