Zana Muhimu
Ni nini kimejumuishwa kwenye Seti yangu ya Starlink?
1. Kuanza Baada ya kufungua Seti yako ya Starlink, inua kiweko na uchomeke ncha moja ya kebo ya Starlink uliyopewa ndani ya Starlink yako. Hakikisha kipengele cha kufunga kebo kimeelekezwa juu na kebo ya Starlink inakaa sawasawa ndani ya Starlink yako.
Kisha elekeza ncha ya pili ya kebo ya Starlink kwenye ruta yako na uichomeke kwenye tundu la 1, kama inavyoonyeshwa na alama ya Starlink nyuma ya ruta huku kipengele cha kufunga kebo kikielekea chini.
Sasa kwa kuwa seti na ruta vimeunganishwa, chomeka kebo ya umeme ndani ya kigawi cha umeme, na ncha ya pili ndani ya ruta.
2. Kusanidi Starlink Starlink yako inahitaji mwonekano wazi wa anga ili iweze kuendelea kuunganishwa na setilaiti zinaposonga juu. Vitu vinavyozuia muunganisho kati ya Starlink yako na setilaiti, kama vile tawi la mti, mlingoti, au paa, vitasababisha ukatizaji wa huduma. Bofya hapa ili kutazama mwongozo wa video kuhusu vizuizi
Ili kupata eneo lenye mwonekano wazi wa anga:
a. Pakua Programu ya Starlink.
b. Tumia zana ya "Angalia Vizuizi" ili kupata eneo la ufungaji ambalo litatoa huduma bora.
c. Kwa matokeo bora, tumia kiweko kuinamisha Starlink
Ikiwa hukupata eneo lenye mwonekano wazi wa anga kutoka ardhini, fikiria kuifunga katika eneo la mwinuko, kama vile paa, ufito au ukuta. Viunzi na vifuasi vya ziada vinaweza kununuliwa kwenye Duka la Starlink.
3. Fungamanisha Starlink na Uunganishwe Seti yako ya Starlink itahitaji kuelekea kwenye mwelekeo sahihi ili kuunganisha kwenye idadi kubwa zaidi ya setilaiti zilizo juu kwa muunganisho thabiti zaidi. Weka Starlink, na uhakikishe kwamba seti imeinamishwa kwa kutumia kiweko. Bofya hapa ili kupata mwongozo wa ziada kuhusu Zana ya Kufungamanisha.
Fungua Programu ya Starlink kwenye kifaa chako. Baada ya kuunganishwa, programu itakuarifu ikiwa unahitaji kuzungusha Starlink yako ili ifungamanishwe vizuri. Bofya arifa hiyo ili kutumia zana, na urekebishe seti yako ili ilingane na picha iliyo kwenye kifaa chako.
Kwa mwongozo wa ziada wa Zana ya Kufungamanisha, bofya hapa Zana ya Kufungamanisha ni nini na nitaitumiaje?
4. Kuunganishwa
a. Unganisha kwenye mtandao wa STARLINK kwenye mipangilio ya WiFi ya kifaa chako.
b. Ili kulinda mtandao wako wa WiFi ya Starlink, tumia Programu ya Starlink ili kubadilisha jina la mtandao wako wa WiFi ya Starlink na kuunda nenosiri la WiFi. Fungua Programu ya Starlink > Mipangilio > Ruta > weka jina na nenosiri la mtandao wa WiFi unalotaka > Hifadhi.
c. Sasa umeunganishwa! Ili kubadilisha mipangilio ya ziada, kuangalia muunganisho wako na zaidi, tembelea Programu ya Starlink.
Mwanga ulio kwenye ruta unamaanisha nini?
Mwanga wa ruta hubainisha hali ya ruta, kama inavyofafanuliwa hapa chini:
Kutumia Matundu ya Ziada ya RJ45 Ondoa kifuniko cha RJ45 nyuma ya ruta, na uchomeke kebo yako mwenyewe ya ethaneti kwenye tundu la 1 au 2. Unganisha ncha ya pili ya kebo yako kwenye zana na vifaa vya wahusika wengine.
Ikiwa bado wewe si mteja wa Starlink: Agiza Sasa*.*
Pata taarifa za barua pepe za Starlink hapa.
Mada Zinazopendekezwa:
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.