
Zana Muhimu:
Tumefanya marekebisho madogo ya muundo kwenye Starlink Mini ili kuifanya iwe yenye kudumu zaidi na ikinze mikwaruzo lakini hayaathiri kazi au utendaji wa Starlink Mini.
Ni nini kinachojumuishwa kwenye Seti yangu ya Starlink Mini?
1. Pakua Programu ya Starlink
Pakua Programu ya Starlink na uchanganue msimbo wa QR ulio kwenye kifurushi cha seti ili upitie mchakato wa kufunga.

2. Tafuta Mwonekano Wazi wa Anga na Uangalie Vizuizi
Starlink yako inahitaji mwonekano wazi wa anga ili iweze kuendelea kuunganishwa na setilaiti zinaposonga juu. Vitu vinavyozuia muunganisho kati ya Starlink yako na setilaiti, kama vile tawi la mti, ufito au paa, vitasababisha ukatizaji wa huduma. Tumia zana ya kizuizi iliyo kwenye programu ili kuhakikisha umechagua eneo linalofaa la kufunga. Bofya hapa ili kuona mwongozo wa video kuhusu vizuizi.

Ikiwa hukuweza kupata eneo la mwonekano wazi kutoka ardhini, fikiria kuifunga katika eneo la mwinuko, kama vile paa, ufito au ukuta. Adapta ya Bomba ya Mini na Kiunzi Bapa kinajumuishwa kwenye seti na viunzi na vifuasi vya ziada vinapatikana kununuliwa kwenye Duka la Starlink.

3. Chomeka Starlink
Starlink Mini ina ruta ya ndani ya WiFi, kumaanisha kwamba ruta tofauti haihitajiki ili uingie mtandaoni. Inua kiweko na uchomeke ncha moja ya kebo uliyopewa ndani ya Starlink yako. Hakikisha plagi imechomekwa kikamilifu ili uso wa plagi uwe sambamba na sehemu ya juu.
Peleka ncha ya pili ya kebo ya umeme kwenye kigawi chako cha umeme na uichomeke kwenye soketi ya umeme.

4. Unganisha kwenye WiFi
a. Kwenye kifaa chako, tafuta na uunganishe kwenye mtandao wa STARLINK katika mipangilio yako ya WiFi
b. Ili kulinda mtandao wako wa WiFi ya Starlink, tumia Programu ya Starlink kubadilisha jina la mtandao wako wa WiFi ya Starlink na kuunda nenosiri la WiFi. Fungua Programu ya Starlink > Mipangilio > Ruta > weka jina na nenosiri la mtandao wa WiFi unalotaka > Hifadhi.

c. Sasa umeunganishwa! Fungua Programu ya Starlink ili uweke upendavyo mipangilio ya ziada, uangalie muunganisho wako na zaidi.
5. Fungamanisha Starlink Seti yako ya Starlink inahitaji kuelekea mwelekeo sahihi ili kuunganisha kwenye idadi kubwa zaidi ya setilaiti kwa muunganisho thabiti zaidi. Funga Starlink na uhakikishe kwamba seti imeinamishwa kwa kutumia kiweko, au tumia Adapta ya Bomba ya Mini na Kiunzi Bapa ulichopewa ikiwa una bomba la ufungaji. Bofya hapa ili upate mwongozo wa ziada kuhusu zana ya kufungamanisha.

Kumbuka: Ikiwa Starlink yako imefungamanishwa ndani ya digrii 5, programu haitakuarifu, ikionyesha Starlink yako imefungamanishwa vizuri.
Starlink Nyingi: Ikiwa unafunga Starlink nyingi katika eneo moja, umbali wa chini wa kutenganisha kutoka katikati ya kiunzi hadi katikati ya kiunzi unapaswa kuwa mita 3. Ruta ya wahusika wengine inaweza kutumika kuunganisha Starlink hizo pamoja kwenye mtandao mmoja na kutoa usawazishaji wa mzigo, kuelekeza trafiki, kuhamishia kwenye njia mbadala, na uwezo mwingine wa hali ya juu.
Je, Umeshindwa Kuingia Mtandaoni?
Fungua Programu ya Starlink ili uangalie arifa, kukatika au vizuizi vyovyote.
Angalia mwangaza wa hali ulio upande wa nyuma wa Starlink yako.
Kumwekamweka Polepole: Imewashwa.
Hakuna Mwangaza: Hakuna umeme kwenye Starlink.
Kumwekamweka Haraka: LED itamwekamweka haraka kwa sekunde 3 wakati unashikilia kitufe cha kuweka upya, kisha LED itazima Starlink yako inapowashwa upya.

Hakikisha kila kitu kimechomekwa vizuri na hakuna uharibifu kwenye zana na vifaa au kebo.
Zima na uwashe Starlink yako kwa kuchomoa plagi kutoka kwenye umeme kisha uichomeke tena.
Rejesha mipangilio ya kiwandani ya Starlink kwa kubonyeza ikoni ya kuweka upya katika upande wa nyuma. Bonyeza kwa uthabiti hadi usikie au uhisi sauti ya kidoko kisha uishikilie kwa sekunde 3. LED itamwekamweka haraka na kuzimika itakapokamilisha. Pitia mchakato wa kufunga ili ufunge Mini yako na uingie mtandaoni.
Starlink Mini inafanya kazi na ingizo la volteji ya 12-48V. Ikiwa unakabiliwa na matatizo unapotumia umeme wa 12V au betri, jaribu kupunguza urefu wa kebo au utumie kebo nene zaidi. Unaweza pia kuboresha utendaji kwa kusambaza umeme kwa volteji ya juu ikiwezekana. Utatuzi rahisi ni kutumia kebo ya USB-C ya Starlink Mini na kigawi cha umeme cha 100W USB-C au Adapta ya Gari ya Starlink Mini.
Kumbuka: Jina na nenosiri la mtandao wako litawekwa upya baada ya kukamilisha kurejesha mipangilio ya kiwandani. Tafuta mtandao wa 'Starlink' wakati wa usanidi na usanidi mtandao wako kwa jina na nenosiri unalopendelea.

Kutumia Ruta ya Wavu au ya Mhusika Mwingine
Ikiwa ungependa kuweka mfumo wa wavu kwa kutumia ruta ya Starlink, unaweza kuunganisha ruta kupitia kebo ya ethaneti kwenye tundu la RJ45 au kuunda mtandao pasiwaya wa wavu. Unaweza pia kutumia ruta yako mwenyewe kupitia tundu la RJ45 katika modi ya mchepuko.
Ili kuunganisha ruta kwenye Mini yako ukitumia waya:

Kumbuka: Tumia Kebo ya Starlink Mini inayopatikana kwenye starlink.com/shop ili kulinda sahani yako dhidi ya uingiaji wa maji. Mini haina tena ukadiriaji wa IP67 inayozuia maji kupenya kwa kebo ya mhusika mwingine ya RJ45.

Ili kuweka ruta ya Gen 2 au Gen 3 ya Starlink kwenye Mini yako bila waya, tafadhali rejelea Ninawezaje kusanidi Wavu wa Starlink? kwa maelezo zaidi.
Ikiwa bado wewe si mteja wa Starlink: Agiza Sasa.
Pata taarifa za barua pepe ya Starlink hapa.
Mada Zinazopendekezwa:
Starlink Mini - Kutatua Matatizo ya WiFi
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.