Vizuizi vya sasa:
- Mpango wa mwaliko kwa sasa unapatikana tu nchini Australia, Brazili, Chile, El Salvado, Meksiko, Nyuzilandi na Marekani.
- Waalikwa watatoa tu miamana kwa usajili wa Makazi na Ughaibuni Bila Kikomo. (Hakuna Huduma za Kipaumbele au Ughaibuni GB50)
- Misimbo ya mwaliko huwekwa kwenye kiwango cha akaunti, si kulingana na idadi ya laini za huduma.
- Seti zilizonunuliwa kutoka kwa muuzaji rejareja au muuzaji hazistahiki mpango wa mwaliko. Tafadhali kumbuka, hakuna muamana utakaotolewa, hata kama kiungo cha mwaliko kilitumiwa wakati wa uamilishaji.
Kama mteja wa Starlink:
- Utapokea barua pepe inayokualika kwenye mpango wa mwaliko. Barua pepe hii itakuwa na kiungo chako cha kipekee (kwa mfano, https://www.starlink.com/?referral=RC-XXXXX-XX).
- Unaweza kunakili na kubandika kiungo hiki au kushiriki kupitia programu ya Starlink.
- Katika programu ya Starlink, chagua ikoni ya 'mtu' kisha "Mwezi bila malipo kwako na yeye".
- Rafiki yako uliyemwalika akinunua kupitia kiungo chako cha mwaliko utapokea arifa kupitia barua pepe.
- Siku 30 baada ya akaunti ya rafiki yako kuamilishwa, muamana wa huduma utatumika kwenye akaunti yako.
- Muamana wa huduma utatumika kupunguza jumla ya ankara yako inayofuata.
Ili kuona ni mara ngapi au kiasi cha muamana wa huduma kimetumika kwenye akaunti yako, unaweza kuingia kwenye akaunti yako kupitia wavuti na uangalie kwenye sehemu ya mwaliko.
Ninawezaje kutumia muamana wangu wa huduma wa mwaliko?
- Kama Mwalikaji (Ulishiriki kiungo chako cha mwaliko): Muamana wa huduma utatumika kwenye akaunti yako siku 30 baada ya mtu uliyemwalika kuamilisha akaunti yake. Baada ya kutumika kwenye akaunti yako, utatumika kupunguza ankara yako inayofuata.
Kwa kushiriki, unakubaliana pia na Sheria na Masharti yaliyobainishwa hapa chini:
- Ili kustahiki zawadi ya mwaliko, mambo yafuatayo lazima yafanyike:
- Mteja aliyealikwa si mteja wa sasa wala hajawahi kuwa mteja wa Starlink;
- Mteja aliyealikwa lazima anunue Seti ya Starlink kwa kutumia kiungo cha kipekee cha mwaliko ulichotoa;
- Mteja aliyealikwa lazima abaki kuwa mteja wa Starlink wa kulipia kwa angalau mwezi mmoja (1) baada ya kuamilisha Seti ya Starlink.
- Mpango huu wa mwaliko unatumika tu kwa matoleo ya Starlink ya Makazi na Ugahibuni ambapo Starlink inapatikana mara moja. Wateja walioalikwa katika maeneo yaliyoorodheshwa kama "Yanasubiri kuorodheshwa" kwenye Ramani ya Upatikanaji hawajumuishwi katika ofa hii: starlink.com/map.
- Starlink inaweza, wakati wowote na kwa hiari yake na bila ilani ya awali, kusitisha, kughairi, kusimamisha au kurekebisha mpango wake wa mwaliko au masharti haya.
- Starlink ina haki ya kuwekea kikomo, kughairi, kuchelewesha au kubatilisha zawadi ya mwaliko ikiwa Starlink itaamua, kwa hiari yake pekee, kwamba mshiriki ametenda kwa njia ya ulaghai au matumizi mabaya au ikiwa Starlink itasitisha au kusimamisha akaunti ya mtumiaji ya Starlink kwa kutegemea ukiukaji wa Masharti ya Huduma ya Starlink.
- Unakubali kutojiwakilisha kama mfanyakazi au wakala wa Starlink, au kama msambazaji au muuzaji wa Seti za Starlink.
- Unakubali kuikinga na kuiondolea hatia Starlink na maafisa wake, wakurugenzi, wafanyakazi na mawakala kutoka kwa na dhidi ya, na unachukua jukumu kamili kwa mashtaka yote ya wahusika wengine, vitendo, madai, hasara, hukumu, fidia, gharama na matumizi yanayotokana na uzembe wako, uwakilishi potofu, ulaghai, hitilafu au kutotenda kunakohusiana na au kuhusu Starlink, Bidhaa zake au Mkataba huu.