Chaguo la kusitisha huduma linapatikana tu kwa mipango ya huduma ya Ughaibuni na Kipaumbele cha Mwendoni. Mipango mingine ya huduma ina chaguo la kughairi huduma na katika maeneo mengi inaweza kuamilishwa tena baadaye.
Jinsi ya kusitisha kupitia tovuti:
- Ingia kwenye akaunti yako katika starlink.com
- Chini ya "Starlink Zako", bofya "Dhibiti"
- Bofya "Sitisha Huduma". Ikiwa chaguo la kusitisha halionekani, basi mpango wako wa huduma haulitumii. Hata hivyo, katika hali nyingi, kipengele cha kughairi na kuamilisha tena hutumika kama usitishaji (kulingana na upatikanaji wa huduma wakati wa kuamilisha tena).
Jinsi ya kuondoa kusitisha kupitia tovuti:
- Ingia kwenye akaunti yako katika starlink.com
- Chini ya "Starlink Zako", bofya "Dhibiti"
- Bofya "Endelea na Huduma"
Maelezo muhimu:
- Ikiwa utasitisha huduma yako kabla ya mwisho wa kipindi chako cha sasa cha bili, bado utapokea huduma kwa kipindi chako kilichobaki cha bili. Unapoanzisha tena huduma yako, ada ya usajili wa kila mwezi itatozwa mara moja, kwa uwiano wa muda uliotumika kulingana na gharama ya mpango kila mwezi na muda uliobaki kwenye mzunguko wako wa bili wa akaunti ulioamuliwa awali.
- Bili za usajili wa Starlink zimefungamanishwa na saa za UTC, kwa hivyo mabadiliko yanahitaji kufanyika kabla ya siku yako ya bili 6:00 usiku UTC ili yaweze kuhesabiwa katika kipindi cha hivi karibuni cha bili.
- Mabadiliko yoyote yaliyofanywa baada ya usiku wa manane yatacheleweshwa hadi kipindi kifuatacho cha siku ya bili, ambacho kitakuwa saa 6:00 usiku saa za UTC kwa siku ya bili mwezi ujao.
Kwa ankara ya kwanza:
- Unaweza kusitisha huduma kabla ya kuamilishwa ili usitozwe kwa ankara ya kwanza. Unaweza kusitisha huduma kupitia ukurasa wa Akaunti yako (kupitia starlink.com) mara tu Starlink yako itakaposafirishwa. Baadaye, bili ya kwanza itatengenezwa wakati utaondoa sitisho/kuamilisha tena huduma yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu wakati uamilishaji unatokea, tembelea Maswali haya Yanayoulizwa Mara kwa Mara.
Ni nini kitatokea ikiwa nitaghairi au kusitisha huduma yangu baada ya siku yangu ya bili/ankara kutengenezwa?
- Ukighairi au kusitisha baada ya siku yako ya bili/ankara kutengenezwa, bado utawajibika kwa ankara ya mwezi huo. Huduma yako itaendelea hadi mwisho wa mzunguko wa sasa wa bili.{
Mada zinazopendekezwa:
Bili inafanya kazi vipi?
Ninawezaje kuamilisha tena huduma?