Inaweza kutumika wakati:
*Vikomo: *
- Uamilishaji wa mpango wa huduma ya Standard na Kipaumbele hauwezekani katika maeneo ambayo nafasi zimejaa kabisa. Unaweza kutazama ramani ya upatikanaji wa huduma ya Starlink kwenye starlink.com/map. Ikiwa nafasi imejaa na hakuna nafasi ya kutoa huduma katika eneo hilo, utakuwa na chaguo la kuamilisha kwa mpango wa huduma wa aina ya Mwendoni.
- Kuamilisha mipango ya huduma ya Standard au ya Mwendoni katika akaunti iliyopo ya aina ya Biashara hakukubaliwi.
- Kuamilisha Starlink kwa matumizi katika nchi tofauti na nchi iliyotumika wakati wa kujisajili mara ya kwanza kwenye akaunti hakukubaliwi.
- Huduma haitaamilishwa kwa Starlink ambazo zimewekwa katika akaunti iliyopo kwa sasa.
*Kumbuka: Kwa wakati huu, akaunti za Brazili na Naijeria haziwezi kuongeza zaidi ya laini moja ya huduma kwa kila akaunti.
- Tumejizatiti kutoa intaneti ya kasi ya juu nchini Nigeria na tunashirikiana kwa karibu na wadhibiti ili kufanya marekebisho ambayo yataboresha huduma kwa wateja. Mpaka mabadiliko haya yaidhinishwe, tunasimamisha maagizo mapya ya Makazi. Weka amana sasa ili uhifadhi Starlink yako na utapokea arifa baada ya maagizo kuanza tena.
Taarifa ya Ununuzi wa Rejareja: Unaponunua seti mpya ya rejareja, utapokea saa moja ya ufikiaji wa intaneti wakati unachomeka kwenye Starlink yako mara ya kwanza. Hii hukuruhusu kuamilisha huduma yako na kukamilisha mchakato wa kujisajili hata bila muunganisho wa intaneti uliopo. Ikiwa utamaliza hiyo saa moja ya ufikiaji, unaweza kuamilisha Starlink yako kwa kutumia chanzo kingine cha intaneti na kufuata hatua za uamilishaji zilizoorodheshwa hapo juu.
Ili kuamilisha Seti yako ya Starlink, fuata hatua hizi:
- Nenda kwenye www.starlink.com/setup
- Pakua programu ya Starlink na ufuate hatua za kusanidi zilizoelekezwa au ubofye "amilisha mtandaoni" ili kuamilisha mtandaoni
- Weka kitambulishi chako cha Starlink
(Mfano wa kitambulishi cha Starlink kilicho kwenye programu ya Starlink wakati umeingia kwenye akaunti yako.)
- Chagua "Akaunti Mpya" au "Akaunti Iliyopo"
- Weka anwani yako ya huduma
- Chagua mpango wa huduma
- Jaza maelezo yako ya mawasiliano na bili
- Bofya "Weka Agizo" ili kuamilisha huduma yako. Taarifa yako ya huduma ya Starlink itatengenezwa kiotomatiki kila baada ya siku 30.
- Ikiwa utakumbana na matatizo yoyote wakati wa uamilishaji, [wasiliana na Kituo cha Usaidizi cha Starlink](https://starlink.typeform.com/to/GRwcMQsD# &source=activation_faq) ili kupata usaidizi.
Mada Zinazopendekezwa:
Kitambulishi cha Starlink ni nini?