Sikupokea Barua Pepe ya Kusanidi Akaunti Yangu
Ikiwa hukupokea barua pepe ya uthibitisho baada ya kuweka agizo lako la kwanza au hujapata barua pepe zozote kutoka Starlink, huenda uliweka anwani yako ya barua pepe ikiwa na kosa wakati wa kujisajili. Jaribu urejesho wa akaunti "kwa simu" ili kuweka upya nenosiri lako. Utaingizwa kwenye akaunti yako, ambapo unaweza kusasisha maelezo yoyote ya akaunti kama anwani yako ya barua pepe.
Umefungiwa Nje/ Umesahau Nenosiri
Je, unakabili matatizo kwenye Uthibitishaji wa Hatua Mbili? Tembelea Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara hapa.
Ikiwa huwezi kuingia mtandaoni, ghafla unajikuta nje ya mtandao au huwezi kufikia akaunti yako; unaweza kupiga simu [1-866-606-5103](simu: 18666065103) nchini Marekani au [1-888-864-1321](simu: 18888641321) nchini Kanada kwa usaidizi wa simu. Kwa sasa huduma hii iko katika awamu ya majaribio na ni kwa wateja wa Starlink tu nchini Marekani na Kanada ambao wanakumbwa na matatizo ya muunganisho. Kwa matatizo mengine, tafadhali wasilisha tiketi ya Starlink. Laini ya simu imefunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa, saa 12 asubuhi hadi saa 10 alasiri Saa za Kati.
Kumbuka: Lazima uwe na nambari yako ya akaunti ili upokee usaidizi wa simu.
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.