Starlink sasa hutoa udhibiti wa ufikiaji unaotegemea jukumu ndani ya tovuti ya Starlink.com (inakuja hivi karibuni kwenye programu ya kifaa cha mkononi ya Starlink). Udhibiti wa ufikiaji unaotegemea jukumu (RBAC) unakupa udhibiti zaidi wa ni nani ndani ya akaunti yako anayeweza kuona taarifa na kufanya mabadiliko. Tumetenganisha kazi tofauti ndani ya Starlink.com na kuziweka katika majukumu tofauti. Kila jukumu lina chaguo la kuhariri na kusoma tu (isipokuwa Msimamizi) na majukumu yanaweza kuunganishwa ili kuendana na mahitaji yako mahususi.
Kwa mteja wa biashara, udhibiti wa ufikiaji unaotegemea jukumu ni kipengele muhimu cha usalama ili timu tofauti ndani ya shirika lako ziweze kuchangamana kwa urahisi huku kila timu ikibaki kwenye majukumu yake. Kwa mteja wa makazi, hii inaweza kukuwezesha kumpa mpangaji au mkazi mwenza katika chumba uwezo wa kuwasha upya kifaa chake au kuanzisha tiketi ya usaidizi bila yeye kuwa na ufkiaji wa kununua seti nyingine ya Starlink, au vifuasi.
Majukumu yanayopatikana yatakuwa:
Msimamizi: Utendaji kamili wa Starlink.com pamoja na uwezo wa kuhariri majukumu; kila akaunti lazima iwe na angalau msimamizi 1
Bili: Uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye vichupo vya bili na duka (fanya malipo, sasisha taarifa za malipo, angalia ankara na salio la akaunti, agiza kupitia duka la Starlink)
Ufundi: Uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye dashibodi na kurasa za laini za huduma (kutatua matatizo na kuchukua hatua kwenye vifaa na huduma yako: dhibiti laini za huduma, chukua hatua kwenye kituo na ruta ikiwa ni pamoja na kuwasha upya, kufungasha, kusanidi Starlink yako, kusasisha sera ya IP, kuongeza/kuondoa starlink, kuongeza laini ya huduma na kubadilisha mpango wa huduma)
Usaidizi: Watumiaji wote wataweza kufikia Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara, lakini jukumu la usaidizi litahitajika kuunda, kutazama na kujibu tiketi za usaidizi
Usimamizi wa Mtumiaji: Ongeza, futa, na uangalie watumiaji na uhariri jukumu/majukumu yaliyokabidhiwa watumiaji
Hapa chini kuna mifano michache ya jinsi majukumu haya yanaweza kutumiwa:
Ni nini ambacho hakijumuishwi katika uzinduzi huu wa awali wa udhibiti wa ufikiaji unaotegemea jukumu?
Mada Zinazohusiana:
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.