Ili kuangalia viwango vya kupakia/kupakua, ubora wa mawimbi, asilimia ya kizuizi na takwimu za ucheleweshaji na upotezaji wa mlio, chagua kichupo cha "Dashibodi" wakati umeingia kwenye akaunti yako. Dashibodi ya Starlink inaboreshwa ili kuwa na ramani ya moja kwa moja ya eneo, inayoonyesha eneo na hali ya vifaa vyako. Sehemu ya juu ya ramani ina jumla ya idadi ya vifaa vilivyo "mtandaoni", "nje ya mtandao" na katika hali ya "hakuna data". "Nje ya mtandao" inamaanisha kwamba kifaa hapo awali kilikuwa kimeunganishwa kwenye mtandao, lakini kwa sasa hakijaunganishwa. "Hakuna data" inamaanisha kwamba kifaa hakijawahi kuunganishwa kwenye mtandao.
Karibu na muhtasari huu kuna jumla ya idadi ya arifa kwenye akaunti. Kwenye kona ya juu kulia kuna kitufe cha kuonyesha upya data ya telemeta kwenye vifaa vyako. Kuna kisanduku cha utafutaji upande wa juu wa ukurasa kilicho na uwezo uliopanuliwa. Utafutaji halisi sasa unaweza kutumika kwa kuweka sehemu nzima katika alama za nukuu. Kwa mfano, ikiwa laini yako ya huduma ina jina la utani '123', unaweza kutafuta "123" ili kuchukua laini hiyo ya huduma pekee.
Utafutaji wa laini ya huduma unaweza kufanywa kwa sehemu zifuatazo:
Orodha ya laini ya huduma upande wa kushoto inaonyesha muhtasari wa hali ya kifaa kwenye kila laini ya huduma na idadi ya arifa kwenye laini hiyo ya huduma. Unaweza kubofya kwenye 'mraba wenye kishale' ili kufungua ukurasa binafsi wa laini ya huduma na kudhibiti laini hiyo ya huduma. Ukibofya kwenye laini ya huduma, ramani itaelekea kwenye eneo hilo kwenye ramani na kutoa muhtasari wa utendaji wa hivi karibuni na arifa zozote amilifu zilizo chini ya skrini. Kwa kutumia ramani, unaweza kuchuja kulingana na hali ya kifaa au kwa arifa mahususi.
Ukichuja ukitumia machaguo yoyote yaliyo upande wa juu wa ukurasa, kitufe cha "Futa Vichujio" kitaonekana upande wa juu wa ukurasa. Vichujio vitasasisha orodha ya laini ya huduma upande wa kushoto ili kuonyesha vifaa vinavyoonyeshwa kwenye ramani. Orodha ya laini ya huduma inaweza kupanuliwa ili kuona muhtasari wa metriki zote za utendaji wa laini ya huduma kwa kubofya kishale upande wa kulia. Katika mwonekano huu uliopanuliwa, unaweza kupanga kulingana na metriki kwa kubofya kichwa cha metriki hiyo, na safu ambayo inapangwa itakuwa na kichwa cha herufi nzito.
Ramani pia inaweza kubadilishwa ili kuonyesha metriki nhyingine ikiwa ni pamoja na asilimia ya kizuizi, kiwango cha kudondosha mlio, ucheleweshaji wa mlio, kiungo cha kwenda juu cha hivi karibuni na kiungo cha kuja chini cha hivi karibuni.
Juu ya orodha ya laini ya huduma, kuna chaguo la "Angalia Laini za Huduma Zisizo na Starlink" ambayo itafungua dirisha linalokuwezesha kutafuta kulingana na nambari ya laini ya huduma au eneo.
Unaweza kujiondoa kwenye ramani ya moja kwa moja ya eneo la akaunti yako ikiwa ni lazima (yaani, Usalama wa Uendeshaji) kwa kuwasilisha tiketi ya usaidizi kwa Kituo cha Usaidizi cha Starlink. Ikiwa umejiondoa kwenye ramani ya moja kwa moja ya eneo, dashibodi itakuwa chaguo-msingi kwenye muhtasari uliopanuliwa wa data ya laini ya huduma kwani ramani itatoa thamani ndogo. Ikiwa ungependa kujisajili kwenye ramani ya moja kwa moja ya eneo, tafadhali wasilisha tiketi ya usaidizi kwa Kituo cha Usaidizi cha Starlink na tutafurahi kukusaidia.
Huwezi kupata kile unachokitafuta? Wasiliana na Kituo cha Usaidizi.